Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (AS) -ABNA- Tamasha maalumu lenye jina la “Hamasa ya Maneno”, msimu wa kwanza wa simulizi za mashairi na fasihi ya Vita Vitakatifu, limefanyika katika Jumba la Makumbusho la Kitaifa la Mapinduzi ya Kiislamu na Vita Vitakatifu kwa ushiriki wa Rahim Makhdomi, mwandishi mashuhuri wa fasihi ya vita.
Katika mwanzo wa hafla hii, Sardar Mahdi Amirian, Mkurugenzi Mtendaji wa jumba hilo, alizungumzia juu ya umuhimu wa mpango huo na kusema: “Wakati wazo la awali la tukio hili lilipowasilishwa kwenye jumba letu na kusomwa, tulilipokea kwa shauku kubwa. Kwa kuwa japo kipaumbele chetu kikuu ni vijana na wanafunzi, mipango ya kitaalamu na ya kiubunifu pia ni muhimu kwetu.”
Akaongeza kuwa: “Kusaidia programu za kitaalamu ni miongoni mwa majukumu yetu, na kwa heshima kubwa tunakaribisha na kuunga mkono matukio kama haya ambayo yanahusiana na uwanja wa Vita Vitakatifu.”
Sardar Amirian alisisitiza kwamba maneno yana uzito, roho na nishati, na yakitoka moyoni huingia mioyoni mwa watu. Aliongeza kuwa: “Sifa kuu ya mpango huu ni mtazamo wake wa kuelezewa na kuenezwa. Tukilichukulia kwa umakini jina la mpango huu – ‘Hamasa ya Maneno’ – basi tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika kukuza utamaduni huu.”
Akaendelea: “Tunafanya kazi kwa ajili ya mustakabali. Hatujafungia historia ndani ya kuta za jumba hili, bali tunaibeba kwa vizazi vijavyo. Vita vya Miaka Minane ni kilele cha historia ya taifa hili kubwa, na kwa ajili ya kuwasilisha urithi wake tunahitaji hamasa ya maneno, simulizi na jihadi ya kuelezewa.”
Katika sehemu nyingine ya hafla hiyo, Reza Maleki, Mkuu wa Mkakati wa Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu, alisema: “Kuvamia ardhi hakuletei ustaarabu, bali ni maadili na kanuni ndizo zinazounda athari za kweli. Vita Vitakatifu vimejaa maadili na kanuni ambazo zinaweza kuwa na thamani za kimataifa kwa sababu zinatokana na maumbile ya Mwenyezi Mungu.”
Maleki aliongeza: “Labda mjadala wa Vita Vitakatifu hautafahamika vizuri nje ya nchi, na vitabu vyetu vikadhaniwa vimefungwa ndani ya mipaka ya taifa letu. Lakini mtazamo huu si sahihi katika mataifa mengi.”
Alibainisha kuwa sehemu ya utambulisho wa Kiislamu, Kiajemi na Kimapinduzi wa Iran umejengwa kupitia Vita Vitakatifu. Kisha akatoa mfano wa jitihada za kueneza fasihi na sinema ya Vita Vitakatifu nje ya nchi akisema: “Katika mradi mmoja nchini Urusi, tulidubua filamu ‘Shiar 143’. Wakati wa onyesho lake la kwanza mbele ya watazamaji 700, wengi waliguswa sana na filamu hiyo na walitoa machozi.”
Maleki alieleza kuwa filamu hiyo baadaye ilioneshwa katika Tamasha la Sinema ya Vita nchini Urusi na kuchaguliwa kuwa filamu bora ya tamasha hilo. Pia, ndani ya muda mfupi, filamu hiyo iliwasilishwa kwenye Tamasha la Filamu la “Nazran” nchini Urusi na kupata nafasi ya kwanza, jambo lililoonesha kuwa malengo yao yalikuwa sahihi.
Your Comment